Online Instagram Content ViewerStalkture
  1. Homepage
  2. itaendelea

#itaendelea photos and videos on Instagram

Medias attached with hashtag: #itaendelea on Instagram

Grandmaster 👑 (MSN) (@mr_celebrityy) Instagram Profile Photomr_celebrityy

Grandmaster 👑 (MSN)

 image by Grandmaster 👑 (MSN) (@mr_celebrityy) with caption : "Video game stuff from @o.dembele7 
Dembele gool 👀

Dream Big! 😀🤙
📲follow @mr_celebrityy ❤️
Follow this  Account plz @mr_" - 1932248342919921487
ReportShareDownload033

Video game stuff from @o.dembele7 Dembele gool 👀 Dream Big! 😀🤙 📲follow @mr_celebrityy ❤️ Follow this Account plz @mr_celebrityy 👥tag friends👇 @neymarjr@mr_celebrityy 🚫IGNORE ➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖➖               #itaendelea 🗽 Tag your friends

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 89 ‘Grace alifariki mwanangu pole sana babaa’ aliniambia
‘whaaaaat! ilikuajeee’" at Dar es Salaam, Tanzania - 1931865290750408787

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 89 ‘Grace alifariki mwanangu pole sana babaa’ aliniambia ‘whaaaaat! ilikuajeee’ nilimuuliza kwa mshangao sababu ya kutoamini alichokisema. ‘mwanangu Grace alifanikiwa kujifungua salama mtoto wa kike ambaye ndiye huyu hapa lakini baada ya kutoka hospitali na kurudi nyumbani kwenu kule mbezi beach alikutana na barua yako juu ya meza uliyomuandikia kuhusu kwenda kwako huko Oman kumtafuta Nairath kiukweli barua hiyo ndiyo ilikua chanzo kikubwa cha kifo chake kwani baada ya kuisoma tu presha ilimpanda akaanguka chini na kupoteza fahamu kitu kilichofanya arudi tena hospitali ambako alilazwa siku 3 na siku ya 4 saa 5 na nusu usiku akaaga dunia pasipo hata kumpa jina mtoto wake.’ mama aliniambia. ‘ni makosa yangu mama, kwa hiyo huyu ni mwanangu’ nilimuuliza. ‘ndiyo ni mwanao kabisa’ mama alinijibu. ‘mmempa jina gani?’ nilimuuliza tena. ‘tuliamua kumpa jina la Nairath kama ishara ya kuwakumbuka nyote’ alisema. ‘Nairaaaath!!?’ nilimuuliza kwa mshangao. ‘ndio anaitwa Nairath mbona umeshtuka’ aliniuliza huku nae akianza kulia. ‘mama Nairath nae amefariki na hawa hapa ni watoto wetu huyu wa kiume anaitwa Javier,na huyu wa kike anaitwa Grace’ Nilimwambia mama yangu huku nikizidi kulia na kumuelezea kila kitu na baada ya kumueleza aliwasogelea na kuwakumbatia huku na mimi kwa mara ya kwanza nikimnyanyua yule mtoto wangu na Grace na kumkumbatia kwa furaha na huzuni nyingi kwa sababu ya jina lake la Nairath kunikumbusha yale yote yaliyotokea kule Oman . baada ya hayo yote mama alitutarishia chakula nika kila na kukimaliza kisha nae kwa mara ya kwanza akaenda kuwaogesha wale wajukuu wake wawili nilioenda nao na kuwanywesha maziwa ya kopo aliyokua akiyatumia yule Nairath mdogo na ghafla akiwa katika kuwanywesha baba yangu mzee Hernandez aliingia ndani akiwa ametoka national stadium kuangalia mpira na baada ya kuingia tulisalimiana akawaona wajukuu wake wapya tukaongea mengi na kisha tukaenda kulala. Nilikuja kuamka majira ya saa 3 asubuhi kwa sababu ya uchovu, nikamsaidia mama yangu kuwaogesha wale watoto wangu #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 88
MTUNZI: FREDRICK LIBENA JAVIER HERNANDEZ ‘kila la heri sitokusahau’
‘mimi pi" at Dar es Salaam, Tanzania - 1931862027145714155

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 88 MTUNZI: FREDRICK LIBENA JAVIER HERNANDEZ ‘kila la heri sitokusahau’ ‘mimi pia sitokusahau kila la heri’ tuliagana. Ilikua ni huzuni kubwa sana katika kuagana kwetu ambapo baada ya kumaliza niliingia mpaka hotelini nikiwa pamoja na wale watoto wangu na nikaanza kupanga mizigo yangu pamoja na kile chumba nilichokikabidhi siku hiyo muda mchache kabla ya kwenda airport kuianza ile safari ya kurejea nyumbani nchini Tanzania. Nilienda mpaka airport pale Musqat mjini nikiwa pamoja na watoto wangu sote tukaingia ndani ya ndege ya Oman airways mali ya serikali hiyo na baada ya kuingia safari yetu ya kuelekea nyumbani nchini Tanzania ikaanza. licha ya ule urefu wa safari pamoja na usumbufu nilioupata kutoka kwa wale malaika wangu wadogo tulifanikiwa kufika na kutua salama juu ya kiwanja cha ndege cha mwl Julias Nyerere na bila kuchelewa nilichukua tax nikapakia mizigo yangu pamoja na wale watoto wangu na safari ya kuelekea nyumbani kwa wazazi wangu ikaanza huku hofu kubwa ikionekana kuuvaa mwili wangu kwa sababu ya kuogopa kupokea taarifa zozote mbaya za Grace pamoja na lawama zilizokua zikisubiri kunishambulia. Tulifika salama mpaka nyumbani kwa wazazi wangu na baada ya kufika kwa wasiwasi mwingi na hofu kubwa niliusogelea ule mlango wa kuingilia sebleni huku nikiwa nimewabeba watoto wangu pamoja na ile mizigo yangu. sikuamini kabisa nilichokiona mara tu baada ya mimi kuingia ndani. Nilimuona mama yangu mzazi akiwa anacheza na mtoto mdogo wa kike ambaye alionekana kufanana sana na Grace. ‘mama mwanao nimerudi naomba unisamehe sana mama’ nilisema huku nikilia na kuwashusha wale watoto wangu kisha nikapiga magoti na kumsogelea. ‘karibu sana mwanangu’ mama alinijibu huku akinikumbatia kwa furaha. ‘asante mama naomba unisamehe sana’ nilimwambia. ‘nisha kusamehe mwanangu’ alinijibu. ‘asante mama vipi Grace yuko wapi’ nilimuuliza kwa hofu kubwa kwa sababu ya kuogopa kunyeshewa mvua ya lawama. ‘Grace alifariki mwanangu pole sana babaa’ aliniambia ‘whaaaaat! ilikuajeee’ nilimuuliza kwa mshangao sababu ya kutoamini alichokisema. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 87 ‘youre not a crime but love is a crime’
(wewe sio muhalifu mapenzi ndio mahal" at Dar Es Salam, Dar Es Salaam, Tanzania - 1931380071677070869

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 87 ‘youre not a crime but love is a crime’ (wewe sio muhalifu mapenzi ndio mahalifu) nilimwambia. Hivyo ndivyo ilivyokua kwani hali ya Nairath ilizidi kua mbaya siku hadi siku yani kila siku ikawa ni afadhali ya jana kitu kilichofanya nikae pale nchini Oman kwa muda wa miezi mitatu huku nikisaidiana na wazazi wake pamoja na yule dereva tax kumuuguza Nairath mpaka siku alipokuja kufariki dunia tarehe 26 mwezi wa 9 siku ya jumatano ambayo kamwe sitakuja kuisahau katika maisha yangu. na baada ya kifo chake niliendelea kukaa pale Oman mpaka arobaini yake ilipopita ambapo kwa shingo upande wazazi wake walikubali kunikabidhi wale watoto wangu ili nirudi nao nchini Tanzania huku wakiomba niwalee na kuwatunza katika maadili mema yampendezayo Mungu. ‘asanteni sana kwa wema wenu nitawalea watoto hawa katika maadili mema’ niliwashukuru huku nikiwaaidi kusaidiana na yule mamdogo wake na Nairath aliyeko masaki katika kuwalea hao watoto wangu. Wao pia walinishukuru sana, wakanitakia kila la heri halafu wakanizawadia na albamu kubwa mbili zilizojaa picha za marehemu Nairath kwa ajili ya kumbukumbu na mwisho tukaagana kwa huzuni kubwa huku wakiniomba isiwe mwisho kwenda tena Oman kuwasalimu na kuwapeleka wajukuu zao kuwasalimia. Na baada ya kuagana nao niliondoka na wale watoto wangu pamoja na yule dereva tax ambaye mpaka wakati huo alikua amekua kama ndugu mpaka Fahud sehemu yalipokuwepo makaburi ambapo baada ya kufika sote tulikwenda moja kwa moja mpaka mahali lilipokuwepo kaburi la Nairath ambalo kwa mara ya mwisho nililiwekea maua pamoja na kumsalia Nairath dua langu la mwisho. ‘kwa heri Nairath kamwe sitakusahau nahaidi nitawalea watoto wetu kama tulivyokua tumejipangia hapo awali katika zile nyakati zetu za furaha pale St.Anna’ nilisema huku nikipiga hatua zangu kuelekea garini na kuianza ile safari yetu ya kurudi hotelini pale Gulf of Oman. Tulifika salama mpaka pale hotelini Gulf of Oman sehemu nilipoagana na yule rafiki yangu dereva tax ambaye alihaidi kunitafuta pindi atakapo rejea nyumbani nchini Tanzania. ‘kila la heri sitokusahau’ ‘mimi pia sitokusahau kila la heri’ tuliagana. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 86  lakini cha ajabu Nairath hakunijibu kitu sababu ya kushindwa kuongea bali al" at Stesheni, Dar-Es-Salaam, Tanzania - 1931370247853708789

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 86 lakini cha ajabu Nairath hakunijibu kitu sababu ya kushindwa kuongea bali aliishia tu kuniangalia mimi pamoja na wale watoto wetu niliokua nimewabeba. sikuweza kabisa kuyazuia machozi yasinitoke baada tu ya kumuona Nairath kiukweli nililia sana sikuataka kuamini kama niliyemuona hapo ndiye yule Nairath niliyeonana nae kule St.Anna university muda mrefu uliopita maana Nairath huyu niliyemuona hospitalini hapo alikua amekonda sana bila huruma vipele viliushambulia mwili wake na kuuharibu sana uzuri wa ile sura yake kwani yale macho yake makubwa meupe ya duara yalionekana kuingia ndani ya sura yake huku zile pua zake nyembamba zikionekana kukonda sana na kubaki mifupa mitupu wakati ile midomo yake iliyokua imezawadiwa lips laini ilionekana kujaa vidonda na kukauka kabisa huku zile nywele zake nzuri nyeusi alizokua akipenda kuzilaza kwa nyumba zikionekana kunyonyoka sana na kua kama kuku aliyenyonyolewa kwenye maji ya moto. Sote tulilia sana hasa yule dereva tax alionekana kulia sana huku akimuomba Nairath msamaha kwa sababu ya kumsababishia mateso yote hayo kwa kumuongezea ile damu yake yenye maambukizi. ‘nisamehe sana binti sikukusudia kabisa kukufanyia hivi’ yule dereva tax alimwambia Nairath huku akilia na kumsimulia kisa kizima jinsi kilivyokua siku ile ambayo Nairath alipata ajali. Maneno yalionekana kumuumiza sana Nairath ambaye naye alianza kulia huku akionekana kuilazimisha ile midomo yake iliyokua imekauka na kujaa vidonda iseme chochote. ‘u.s.i.ja.l.i ni.me.ku.s.amehe.. i.li.k.u.a ni .kwa..a.j.i.li .yangu’ Nairath alimwambia kwa shida kwa sababu ya maumivu ya vile vidonda vilivyokua vimeushambulia mdomo wake bila huruma na kisha baada ya kumwambia yule dereva tax Nairath aliinita kwa shida tena. ‘Javier na.ku.pe.nda s.an.a, na.o.mba .u.nisa.me.he kabla s.ijafa’ Nairath alinambia. ‘nikusamehe kwa lipi wakati mimi ndiye niliyekukosea tafadhali naomba usiseme hivyo wewe haufi Nairath’ nilimwambia. ‘Javier ni.liku.ku.bali a.ngali ,nili.jua .kua nimea.th.i.ri.ka ni.kwa.sababu n.ili.ku.a na.kup.enda .sana..ndi.o. maana nilishind.w.a ku.ku.ambia. ukweli.’ aliniambia. #itaendelea ’

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 85 ‘hakustahili kufa sababu alikua bado binti mdogo sana’ yule dereva tax alisem" at Stesheni, Dar-Es-Salaam, Tanzania - 1931323526503389293

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 85 ‘hakustahili kufa sababu alikua bado binti mdogo sana’ yule dereva tax alisema. ‘tutauamini vipi kama kweli haukukusudia?.’ Mzee Fa-thiya alimuuliza ‘sikukusudia kabisa ndio maana baada ya tukio hilo nilijiwajibisha mimi mwenyewe kwa kuacha kazi na kua dereva tax huku nikiamini siku moja katika mizunguko yangu nitaweza kuonana na binti huyo ili niweze kumuomba msamaha juu ya kile niliyomfanyia lakini nilizunguka karibu miji yote ya hapa Oman pasipo kumuona ma mdio maana nimeshindwa kujizuia kujisema hapa ili miweze kusamehewa na kuitubu dhambi hii iliyonitesa na kunitafuna kwa muda mrefu sana’ alisema. Sote hatukumjibu chochote bali tuliishia kumuangalia kwa macho yenye hasira na huzuni nyingi hakuna hata mmoja kati yetu aliyetambua thamani ya ule wema wake alioutenda wala uzito wa yale machozi yake yaliyokua yakimdondoka na kukisindikiza kile kilio chake kikubwa cha uchungu kwani wote tuliishia kumhukumu ingawa kiukweli alikua ametenda wema mkubwa ulioyasogeza maisha ya Nairath kufikia mpaka muda huo aliokua amelazwa pale hospitalini Good health. ‘haijalishi umetenda wema kiasi gani kamwe hatutokusamehe mpaka pale binti yetu atakapo kusamehe yeye mwenyewe ndipo nasi tutakusamehe’ mzee Fa-thiya alisema. Na baada ya maongezi hayo mazito yenye kuumiza sana safari ya kuelekea hospitalini Good health kumuona Nairath ilianza huku ile kesi yangu pamoja na makosa yangu yote niliyotenda yakionekana kuamia juu ya yule dereva tax. haikua safari ndefu sana kwani baada ya mwendo wa karibu dakika 10 tulifanikiwa kufika salama mpaka pale hospitalini Good health na kisha tukaanza kupiga hatua huku nikiwa nimewabeba watoto wangu kuelekea sehemu ilipokuwepo wodi aliyokua amelazwa Nairath ambapo baada ya mwendo wa kama dakika 2 na nusu hivi tuliifikia wodi hiyo. ‘Nairaaaaaaaaaath!!!! nimekuja hapa kwa ajili yako’ nilisema mara tu baada ya kuingia wodini na kumuona Nairath akiwa amelala kisha nikamkimbilia na kumkumbatia nusura ya kuwaangusha wale watoto wetu. lakini cha ajabu Nairath hakunijibu kitu sababu ya kushindwa kuongea bali aliishia tu kuniangalia mimi pamoja na wale watoto wetu niliokua nimewabeba. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE)84

Mimi ndiye niliyemuongezea binti yenu damu yenye maambukizi…. Ilikua ni siku " at Stesheni, Dar-Es-Salaam, Tanzania - 1931320162495466688

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE)84 Mimi ndiye niliyemuongezea binti yenu damu yenye maambukizi…. Ilikua ni siku ya jumatatu tarehe 23 mwezi wa 10 mwaka 2006 siku nilipokua daktari wa zamu katika hospitali ya Wadi Muqshin ambapo majira ya saa 2 na nusu usiku binti mmoja mwenye umri wa kati ya miaka 19-20 aliletwa akiwa amezirai huku akionekana kupoteza damu nyingi sana kwa sababu ya yale majeraha aliyokua nayo ambayo yalitokana na ajali mbaya ya gari baada ya kumpokea mimi pamoja na timu yangu tulimpeleka mpaka katika chumba cha upasuaji kwa ajili ya kumsafisha yale majeraha pamoja na kuyashona.’ yule dereva tax alisema. Na baada ya kumfikisha katika chumba cha upasuaji kitu cha kwanza ilikua ni lazima tumuongezee damu na hapo ndipo matatizo yalipoanzia maana damu zote za group 0 zilikua zimeisha katika bank ya hospitali hiyo kitu kilichofanya mimi pamoja na wale madaktari wenzangu tupime damu zetu na ndipo damu yangu ikaendana na damu ya binti yenu lakini nilisita kabisa kumuongezea damu yangu maana nilijua wazi kua nilikua nimeathirika. ‘hebu muongeze damu tusipofanya hivyo ni lazima atakufa’ madaktari wenzangu waliniambia. ‘najua kua atakufa lakini mimi ni muathirika’ niliwajibu. ‘wewe ni daktari lazima ujue thamani ya uhai wa mgonjwa wako hebu muongezee tu maana inaweza kuusogeza uhai wake hata miaka 5 mbele huoni ni afadhali kuliko akifa hapa’ waliniambia. Yale maneno ya madaktari wenzangu yalifanya nimtazame kwa huruma yule binti aliyekua ameletwa pale hospitalini na wasamaria wema akiwa amezirai kitu kilichopelekea kufanya yale maamuzi magumu ya kutoa damu yangu yenye maambukizi na kumuongezea ili kuyaokoa maisha yake yaliyoonekana kuelekea ukiongoni na hapo ndipo nilipoamua kutoa damu yangu yenye maambukizi na kumuongezea’ yule dereva tax aliyasema yote hayo huku akilia kama mtoto mdogo mbele ya wazazi wake na Nairath angali akiwa bado amepiga magoti. ‘si bora ungeacha binti yetu afe kuliko anavyoteseka hivi sasa’ mama Nairath alimwambia huku na yeye akilia kwa sababu ya ule upendo na uchungu wa kimama. ‘hakustahili kufa sababu alikua bado binti mdogo #itaendelea

Vyombo & home essentials (@bnbhomeessentials) Instagram Profile Photobnbhomeessentials

Vyombo & home essentials

 image by Vyombo & home essentials (@bnbhomeessentials) with caption : "Lakini pia ukikosa ur dream job usisite kufanya kazi yeyote ilimradi inalipa zingatia yafwatayo kazi ni daraja la kufiki" - 1931161678496303163
ReportShareDownload1367

Lakini pia ukikosa ur dream job usisite kufanya kazi yeyote ilimradi inalipa zingatia yafwatayo kazi ni daraja la kufikia malengo yako kupitia kazi malengo yako yatatimia, kazi ni sehemu ya ww kujifunza so usivunjike moyo ukikosa kazi ya profession yako mfano ww ni banker umepata kazi customer service take it as place for you to learn new skills ipo siku uzoefu wako wa customer service utakufaa kny career yako so brothers and sisters kuajiriwa sio dhambi wengi tumesoma ili tupate our dream jobs so get it I wish you all the best 2. BIASHARA Wapo ambao wamesoma ila wanandoto ya kujiajiri, well n good go ahead my brothers and sisters. Ni kweli biashara zinalipa kama unapenda kufanya biashara ni vizuri sana. Ila please dont copy na kupaste kama zile assignment tulizokua tunagoogle 😁😁 mfano unadoto ya kuuza chakula kama flan go ahead flan hawezi ku feed the whole of Dar ila unapofanya biashara kama ya fulani usifanye kwa lengo la kumuumiza flani. Fanya kwa kua unapenda kile kitu ongeza ubunifu wako the key is learn from your competitors but dont copy yani ukimcompy competitor thats your grave uza chakula kama yy find your own recipe buni majina yako n.k thats the key Ila pia ukiamua kufanya biashara ufunge mkanda sio kitu rahisi you must be flexible na mwanzoni unaweza jikuta unafanya kazi hata 16_20hrs a day biashara ni kama mtoto unatakiwa umlee umkuze, umfunze n.k biashara ina hitaji nidhamu ila ukiifanya vyema biashara is very rewarding chukulia biashara yako kwa umakini uwe tayari kujifunza hudhuria mafunzo mbali mbali jifunze kutoka kwa wapinzani jifunze kutoka kwa wateja usiache kujifunza na usikate tamaa #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 82  baada ya kuwashukuru niliwaomba ruhusa ya kwenda kumuona binti yao kama uli" at Dar es Salaam, Tanzania - 1930392714312409419

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE ) 82 baada ya kuwashukuru niliwaomba ruhusa ya kwenda kumuona binti yao kama ulivyokua ule utaratibu wa pale hospitalini Good health kua ni lazima upate ruhusa kutoka kwa ndugu wa karibu wa mgonjwa ndipo uweze kumuona lakini cha ajabu walinikatalia. nilishangazwa sana na majibu yao ya kukataa mimi nisiende kumuona Nairath kusema kweli wazazi wake na Nairath walinishangaza sana kwani pamoja na kuwabembeleza sana tena kwa machozi bado walitia ugumu kunielewa, niliumia sana kwani licha ya kuwaambia ukweli wote na kuthibitisha wazi kua nina mpenda sana binti yao bado hawakunielewa hata kidogo na hawakutaka kusikia kabisa hiyo habari ya kuongozana nao hospitali. ‘kwanini hamtaki kuniruhusu’ niliwaliza kwa wasiwasi mwingi. ‘nadhani inatosha kuwaona watoto wako tafadhali muache binti yetu afe kwa amani’ mzee Fa-thiya alinijibu. Majibu yake yenye utata mwingi, yalifanya maswali mfululizo yasiyokua na majibu yaushambulie ufahamu wangu kwani nilibaki nimeduwaa huku nikishindwa cha kufanya. ‘kwanini afe? kwani hali yake ikoje na anasumbuliwa na nini’ niliuliza. ‘Javier, inaniuma sana huwezi kuamini kua Nairath ni muathirika wa virusi vya ukimwi’ mama yake na Nairath aliniambia huku akilia kwa huzuni. ‘whaaaaat!!! Nairath ni muathirika?’ niliuliza kwa mshangao. ‘ndio ni muathirika tena wa muda mrefu sana’ aliniambia huku akizidi kulia. ‘mama hebu niweke wazi mbona sikuelewi’ nilimuuliza tena kwa kutahamaki. ‘najua utaumia sana lakini hatuwezi kuubadilisha ukweli Nairath ni muathirika toka mwaka 2006 alipokua na umri wa miaka 19 alipata ajari mbaya sana ya gari na ndipo tulipomkimbiza hospitali na katika haraka ya kuyaokoa maisha yake inasadikika aliongezewa damu yenye maambukizi kutoka kwa mtu asiyefahamika kwa sababu damu zote zilizokuwepo kwenye bank ya hospitali hiyo hazikuendana na group la damu ya Nairath’ mama yake aliniambia. Yale majibu hayakuishia kunihuzunisha tu bali yalinikatisha sana tamaa ya maisha nilijua wazi kua ni lazima nitakua nimeathirika nililia sana na kwa mara ya kwanza nikayaamini maneno ya wahenga kua si kila king’aacho ni dhahabu vingine ni adhabu. #itaendelea

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) Instagram Profile Photostorynzuriiplanet

Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹

 Instagram Image by Shaaban Habibu🇹🇿🇰🇪🌹 (@storynzuriiplanet) with caption : "STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 81

MTUNZI: FREDRICK LIBENA 
wazazi wake na Nairath walinielewa lakini hawakua t" at JWTZ Military Base Lugalo - 1930271421692872679

STORY: NISAMEHE GRACE(FORGIVE ME GRACE) 81 MTUNZI: FREDRICK LIBENA wazazi wake na Nairath walinielewa lakini hawakua tayari kunisamehe kabisa kwa sababu waliniona kama muuaji na mtu niliyeyaharibu sana maisha ya binti yao huyo na kufanya ashinwe kutimiza malengo yake aliyojiwekea. ‘sidhani kama tutakusamehe naamini hata Nairath pia hatoweza’ aliniambia. ‘haijalishi, ninachohitaji ni kumuona tena na kuwaona watoto wangu’ niliwajibu. Hakuna mtu aliyenisemesha wala kunijibu tena mara baada ya kuwaambia hayo maneno kwani ukimya ulitawala kwa dakika kadhaa na ghafla yule binti aliyetufungulia mlango hapo awali aliwanyanyua watoto wangu na kuwasogeza mpaka kwangu sehemu nilipokua nimekaa na yule rafiki yangu kwa mara nyingine nikawakumbatia na kuwabusu. watoto wangu walianza kulia baada tu ya mimi kuwashika na kuwakumbatika kiukweli kilio chao kiliniumiza sana kwa sababu sio kwamba walikua wakilia kwa ajili ya utoto wao bali walilia kwa sababu ya sura yangu kua ngeni machoni kwao na kutonifahamu mimi kitu kilichosababisha nafsi yangu izidi kuumia na kunisuta zaidi kwa kuwakosesha wale watoto mapenzi ya kibaba toka walipokua tumboni mwa Nairath hadi hapo walipofikia. Licha ya kulia kwao sikutaka kuwaacha bali niliwabembeleza huku nikizitazama sura zao za kitoto zilizokua za kupendeza sana kwa sababu ya ule uzuri wa rangi nyeupe waliyoichukua kwa Nairath huku yule mtoto wa kike akionekana sana kufanana na mama yangu mzazi kwa sababu ya kufanana sana na mimi wakati yule wa kiume akionekana kufanana sana na Nairath ambaye mpaka muda huo alikua hospitalini. ‘hongera kaka ni wazuri mno’ yule rafiki yangu aliniambia huku akiwatazama. ‘asante nashukuru sana’ nilimjibu. Niliwashukuru sana wazazi wake na Nairath kwanza kwa sababu ya kuulea ule ujauzito wangu aliokuja nao binti yao wakati alipoondoka Tanzania na kuniachia ile barua pili nliwashukuru kwa wema wa kuwalea wale watoto wangu ambao ilikua ni jukumu langu kuwalea wote wao pamoja na mama yao Nairath. na baada ya kuwashukuru niliwaomba ruhusa ya kwenda kumuona binti yao kama ulivyokua ule utaratibu wa pale hospitalini Good health kua ni lazima upate ruhusa kutoka kwa ndugu wa karibu wa mgonjwa #itaendelea